Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

"Inaunganisha Tanzania na Dunia "
TAA Logo

Huduma za Mizigo

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

Huduma za Mizigo

Huduma za Mizigo
Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro una jengo kubwa zaidi la kuhifadhia mizigo katika ukanda wa Kaskazini. Jengo hili lina uwezo wa kutunza bidhaa na mazao yaliyohitaji ubaridi bila kuharibika, na linakidhi vigezo vya IATA huku likiwa chini ya ulinzi kwa saa 24. Jengo hili limegawanyika katika maeneo mawili makuu; jengo la ubaridi na jengo la mizigo kavu.

Jengo la mizigo kavu lina ukubwa wa mita za mraba 110, wakati jengo la ubaridi lina uwezo wa kuhifadhi mizigo yenye uzito wa tani 80. Jengo hili lina huduma zote zinazohitajika kwa usafirishaji wa mizigo kuingia na kutoka nchini, ikiwemo huduma za kuhudumia mizigo, ushuru wa forodha, eneo la maegesho ya malori, na eneo maalumu la kuhifadhia bidhaa hatarishi.

Makampuni yanayosifika katika huduma za usafirishaji duniani kama vile DHL na Kuehne & Nagel yana ofisi katika jengo hili. Mazao yanayosafirishwa zaidi kutoka katika jengo hili ni pamoja na maharage, maua, madini, kahawa, mbegu, na parachichi kwenda nchi za Ulaya, Asia, Mashariki ya Mbali, na Mashariki ya Kati