Usafiri wa Umma
Usafiri wa umma unapatikana kwa kuingia na kutoka Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro. Kituo cha basi kinapatikana baada ya geti la kuu la kuingilila uwanjani, wasafiri wanaotoka na kuingia kiwanjani kuelekea Moshi na Arusha wanaweza kutumia usafiri huu. Msafiri atapaswa kupanda hadi KIA Junction ambapo atapata basi lingine kuelekea Moshi (kilometa 30) na Arusha (kilometa 40).